Sunday, January 22, 2006

CHETI-CERTIFICATE

Mwisho wa hatua ya kielimu na kimaarifa huwa ni cheti.ki kigezo na hati halali ya utambulisho na sifa kuwa unajua kitu hicho. ukimaliza bila kuwa nayo huwezi kujengwa kwa mawazo mema.Mtu hapimwi anajua kwa sababu anauwezo wa kujieleza, kwa sababu ana cheti.Cheti jujenga matabaka, hujenga kiburi na kujiamini. Hujenga heshima na kutambulika.

Cheti ni karatasi tu lililorembwe na kupendeza likiwa na maneno ya kuvutia na kutia mshawasha.hukumbushia madhila ya safari ya kutafuta maarifa, elimu. hukumbushia furaha na nyakati nzuri za marafiki wa zamani, wakati mwanana wa ujana au uzee au utoto. Ni kumbukumbu ya mafaanikio na hatua mbele katika ulimwengu wa elimu.waswahili husema elimu ni bahari.hivyo cheti ni ufukwe wa bahari.unasimama ufukweni na kuangalia bahari kubwa usioona mwisho wake.Kwa ushujaa wa kuvuka salama unakabidhiwa cheti.

Ni alama na maneno ya mibaraka kwa mhusika.ni heshima anayotembea nayo mtu. Ni ukweli uliomo moyoni na kichwani mwa mhusika.Ni tangazo la biashara na kwa sababu chema chajiuza na kuepusha msomi huyu kujiuza akaonekana ni kitu kibaya, cheti kinamuuza.

Cheti ni nabii, ni mtayarishaji wa njia kwa masihi.mwenye cheti ni masihi.cheti hutayarisha mapito ya anaekuja asionekane hana shaidi.

Cheti ni mpambe, ni mtambulishaji halali na aliyekubuhu wa mhusika.hupunguza mfalme kuongea zaidi.ni msemaji wa idara ya moyo wa binadamu.

Cheti ni alama ya ushindi.kwa bahati mbaya cheti kikiungua na huwezi kupatabkingine unauza uhuru, heshima, alama, na unamtoa Nabii kwa wauaji na wasaliti.cheti ni alama ya mwisho ya ujasiri wa mhusika.
Cheti ni muhtasari wa habarui nzima ya binadamu.ni namna ya kujipamba.

Cheti ni dibaji ya kitabu chema, ni suranjema ndani ya kitabu cha kurasa tatu.ni Shuhuda wa kesi na mtetezi wa mdai.

Cheti hukosa uhai mhusika anapokufa, kufungwa maisha.hubaki hakishuhudii.
Elimu inayoshuhudiwa na cheti hufa baada ya cheti kufa au mwenye kushuhudiwa na cheti kufa.

Lakini fikra ipo wapi?fikra haipo kwenye cheti, hapa najua Jeff ataniunga mkono.Fikra haishuhudiwi wala haitambulishwi na cheti, fikra haina shuhuda.Fikra haifi.Mwenye fikra akifa ataiacha fikra ikiishi.Fikra inarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.Elimu hirithishwi.elimu hupewa .Fikra pevu na zao la fikra pevu husumbua moyo, hukereketa kizazi hadi kizazi.
Fikra ni urithi adimu duniani.hupindua falme na miasha ya watu.
Fikra haina shuhuda wa cheti.mwenye kushuhudia fikra ni jamii. na jamii itasambaza hiyo fikra.

Fikra ni fasihi simulizi. ni zao la akili na unga,vu wa akili, lakini elimu ni zao la fasihi andishi. elimu ni mali ya mwenyecheti. si mali ya jamii. ili elimu iwe mali ya jamii mwenye cheti hana budi kuwa na fikra
fikira huokoa.huuisha nafsi. Fikra ni zao la maendeleo ya jamii.

3 Comments:

Blogger Boniphace Makene said...

Bwire unaimba kiriwaya kama malenga wa wimbo ulio bora. Hicho cheti kaka kila mmoja anakikimbilia akidhani ndio mwisho wa reli. Sasa hivi jamii inaona umuhimu wa kuwa na fikra na maarifa sadifu na upungufu kanganyifu unaoletwa na madhila ya elimu vyeti. Safari muhimu na bora kwa binadamu kupita ni hii ya kupata maarifa angavu yavukayo mipaka ya vyeti. Kama unataka weledi utaupata vitabuni. Karibu mwanafikra mpya, wewe mwanazuo kwelikweli pia.

11:31 AM  
Blogger Fikiri said...

bwana fikra kwa kweli wewe ni mwanazuoni nambari wani.
naomba tuwasiliane kwenye email hii (pmapendo@gmail.com) asap.

2:25 AM  
Blogger Innocent said...

Baba umenena, watanzania hawayajui haya, wengi wanadhani cheti mali sana kumbe fikra baba.

Cheti kingekuwa mali unadhani BAlali, karamagi wangekuwa wafisadi?Ni ukosefu wa fikra.
Hongera sana.

4:55 AM  

Post a Comment

<< Home