Sunday, January 22, 2006

CHETI-CERTIFICATE

Mwisho wa hatua ya kielimu na kimaarifa huwa ni cheti.ki kigezo na hati halali ya utambulisho na sifa kuwa unajua kitu hicho. ukimaliza bila kuwa nayo huwezi kujengwa kwa mawazo mema.Mtu hapimwi anajua kwa sababu anauwezo wa kujieleza, kwa sababu ana cheti.Cheti jujenga matabaka, hujenga kiburi na kujiamini. Hujenga heshima na kutambulika.

Cheti ni karatasi tu lililorembwe na kupendeza likiwa na maneno ya kuvutia na kutia mshawasha.hukumbushia madhila ya safari ya kutafuta maarifa, elimu. hukumbushia furaha na nyakati nzuri za marafiki wa zamani, wakati mwanana wa ujana au uzee au utoto. Ni kumbukumbu ya mafaanikio na hatua mbele katika ulimwengu wa elimu.waswahili husema elimu ni bahari.hivyo cheti ni ufukwe wa bahari.unasimama ufukweni na kuangalia bahari kubwa usioona mwisho wake.Kwa ushujaa wa kuvuka salama unakabidhiwa cheti.

Ni alama na maneno ya mibaraka kwa mhusika.ni heshima anayotembea nayo mtu. Ni ukweli uliomo moyoni na kichwani mwa mhusika.Ni tangazo la biashara na kwa sababu chema chajiuza na kuepusha msomi huyu kujiuza akaonekana ni kitu kibaya, cheti kinamuuza.

Cheti ni nabii, ni mtayarishaji wa njia kwa masihi.mwenye cheti ni masihi.cheti hutayarisha mapito ya anaekuja asionekane hana shaidi.

Cheti ni mpambe, ni mtambulishaji halali na aliyekubuhu wa mhusika.hupunguza mfalme kuongea zaidi.ni msemaji wa idara ya moyo wa binadamu.

Cheti ni alama ya ushindi.kwa bahati mbaya cheti kikiungua na huwezi kupatabkingine unauza uhuru, heshima, alama, na unamtoa Nabii kwa wauaji na wasaliti.cheti ni alama ya mwisho ya ujasiri wa mhusika.
Cheti ni muhtasari wa habarui nzima ya binadamu.ni namna ya kujipamba.

Cheti ni dibaji ya kitabu chema, ni suranjema ndani ya kitabu cha kurasa tatu.ni Shuhuda wa kesi na mtetezi wa mdai.

Cheti hukosa uhai mhusika anapokufa, kufungwa maisha.hubaki hakishuhudii.
Elimu inayoshuhudiwa na cheti hufa baada ya cheti kufa au mwenye kushuhudiwa na cheti kufa.

Lakini fikra ipo wapi?fikra haipo kwenye cheti, hapa najua Jeff ataniunga mkono.Fikra haishuhudiwi wala haitambulishwi na cheti, fikra haina shuhuda.Fikra haifi.Mwenye fikra akifa ataiacha fikra ikiishi.Fikra inarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.Elimu hirithishwi.elimu hupewa .Fikra pevu na zao la fikra pevu husumbua moyo, hukereketa kizazi hadi kizazi.
Fikra ni urithi adimu duniani.hupindua falme na miasha ya watu.
Fikra haina shuhuda wa cheti.mwenye kushuhudia fikra ni jamii. na jamii itasambaza hiyo fikra.

Fikra ni fasihi simulizi. ni zao la akili na unga,vu wa akili, lakini elimu ni zao la fasihi andishi. elimu ni mali ya mwenyecheti. si mali ya jamii. ili elimu iwe mali ya jamii mwenye cheti hana budi kuwa na fikra
fikira huokoa.huuisha nafsi. Fikra ni zao la maendeleo ya jamii.

BARA LA GIZA

Isitoshe imekuwa ikinikera muda mrefu, kile kinachoitwa bara la giza , bara la Afrika.Kwa nini lilitwa hivyo na watu wa kaskazini mwa dunia.Jina la kejeli na lenye kila aina ya mzaa. labda kuzarau kilichokuwa Afrika au kwa vile watu wake inasemekana walikuwa wajinga kwa misingi ya akina mangungo wa msovero na kwingineko. Lakini somo la historia na kwenye vitabu dhalilishi vya historia ya maendeleo ya binadanu imebakia hivi kuwa Arika lilikuwa bara la giza.

Kwa misingi kwamba halikujulikana sana na watu wa kaskazini na kuwa shughuli za maendeleo ya binadamu yalikuwa nyuma sana. watu waliishi mapangoni, kwenye nyumba za full suti ya udongo ambazo bado zipo leo Afrika.

Au kwamba waliotumwa kutafuta unafuu wa makazi kwenye dunia isiyojulikana kama Amerika na Afrika waliwakuta watu wa maeneo hayo hawajui chochote kuhusu mabadiliko ya kijamii na kisayansi.Huenda ni kweli kwani akina Williamsoni wa Mwadui shinyanga walikuta wasukuma wa Tanzania wanachezea almasi, akaenda kwao Uingereza na kuja na groli za kuchonga na kubadilishana na almasi zilizotunzwa na wenyeji hao.

Williamsoni alikuwa maskini na kutoka ukoo maskini, baada ya kutajirika akataka kuoa kutoka ukoo wa malkia , lakini alikataliwa kutokana na historia yake, familia yake ilikuwa maskini tu. Akarudi Tanzania , akabadilisha maisha ya mwadui.Ilikuwa sehemu ndogo ya Tanzania yernye kila huduma.Wafanyakazi walipatiwa kila kitu, mkate, mayai, kilo mbili za nyama, mchele, bia , soda na mengine mengi hata maisha yalipobadilika watu hawa leo ni maskini.Hawakuweka akiba , walijua maisha ndo hayo hayatabadilika. imebakia historia nzuri ya kula mayai na mikate.

Wazungu walipora utajiri wetu.Juzi nilikuwa kwenye mji mdogo wa Geita mkoani mwanza kaskazini mwa Tanzania, nilikutana na rafiki yangu mmoja .Tuliongea mengi lakini mwishowe aliniuliza unajua maana ya jina hili GEITA.Nikamwambia hapana. Akanambia kuwa geita ni neno la kizungu.Hapo mgodi wa dhahabu wa geita upo leo wazungu waingereza walichimba zamani na wakagundua kuwa eneo lote la wilaya hiyo ni dhahabu tupu, wakaamua kuliita ''Gold Environment in Tanganyika'' kwa kifupi GEITA. akazidi kunambia kuwa dhahabu ya geita ndo imependezesha London.

Lakini napata hamasa kuu ya kuwa bara la giza lilizipamba Ulaya. Misaada inayopatikana kutoka ulaya ni ziada na faida ya mtaji kutoka Afrika.Viongozi wa Afrika wanapoenda Kaskazini kuomba misaada, siyo misaaada ni kuomba sehemu ya faida ya mtaji wetu ulioporwa.

Nahitaji kuungwa mkono hapa au kupingwa kuwa lazima Afrika leo iwe na hisa katika IMF na WB kwani uchumi wake uliporwa na wazungu kwa lugha isiyo na haya naweza kusema waliiba utajiri Afrika wakitumia ukarimu wa babu zetu.

Afrika halikuwa bara la giza na wala haijawahi kutokea hivyo.Siku zote kaskazinin hutafuta maneno na misamiati ya kupumbaza waafrika.Afrika imekuwa ikikua kwa kasi ukweli ni kwamba mtoto Afrika alichelewa kukua kwa sababu alidekezwa sana na wazazi wake na kwamba walikuwa matajiri kupindukia, hivyo hakuwa na haraka ya kukimbia kimbia ajitegeee
na kuwahi kutafuta mali. Mtoto Ulaya aliwahi kutembea sana, ilikuwa hivyo kwa sababu ya matatizo yake , alikuzwa hivyo ili ajitegemee mapema maana mazingira yake yalikuwa magumu.Hakuwa na ardhi kubwa na pana, yenye rutuba nk.Hivyo kwa ukorofi wake akamwibia ndugu yake Afrika na kuanza kumwuita mjinga na eti yuko gizani.

Mali ya duni a ni ya wote.Lakini linalonishangaza ni kuwa mpaka leo waafrika tunapigana, hatupendani, serikali hazisaidii watu wake, viongozi wetu wanaenda parisi club, IMF,WB na kwingineko kuomba msaada.Wanawaita wawekezaji kuchuma na kuendeleza Waafrika, wanaambiwa ili kuwa na msaada lazima kuwe na utawala bora, haki za binadamu, uwazi kana kwamba sisi bado tuko gizani. La kunishangaza tunaitikia tu kwani tukikataa tutanyimwa misaada.

Ukikataa masharti ya kaskazini unawekewa vikwazo vya kimataifa, vikwazo vya kiuchumi.Ni nini tumemkosea Mungu sisi Afrika na waafrika kwamba uchumi uliojenga ulaya ulitoka Afrika lakini sisi sasa wenye uchumi huo hatuwezi kuutumia kubadilisha maisha na mustakabali wa waafrika wote?Nani au mzazi gani wa Afrika alitenda dhambi hii kubwa ambayo haiwezi kusamehewa nasi tukajenga kujiamini na kizazi hiki kikasomga mbele kwa mbwembwe kama ambavyo kaskazini ilivyo? kwa nini hatuwezi.

Twahitaji kuona ulaya ikija afrika kuomba mali ya Afrika na siyo kuja kutawala Afrika kwa misingi ya mashirika ya fedha n.k

Nitazidi kukataa na kushawishika kuwa Afrika hakuna giza- na wala haijatokea hivyo badala yake giza la ulaya walilileta Afrika na kufanya afrika itiwe huzuni na kubakia hivyo mpaka leo.
Afrika ni mwanga na imekuwa nguzo ya kiuchumi ya dunia mpakam sasa ,Je ni kwa nini tusijenge na kujenga historia yetu ya matumaini kuliko hii ya ulaya ya giza ?
ni wapi lilitendeka kosa?

Tuesday, January 17, 2006

SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU

Nilipozaliwa miaka mingi iliopita, sikujua ni wapi naelekea na ni wapi natoka. ningali mdogo niliiona dunia nzuri sana maana ilikuwa dunia isyokuwa na majukumu, badala yake mimi nilikuwa naidai dunia, maana ilikuwa ni lazima nile, nivae, nilale kuzuri, nitibiwe, nisome au nisomeshwe, nipendwe na watu wangu kunijali kama mtoto na ndugu yao mpendwa.

Nilikuwa zao jipya duniani, mali mpya mnadani na mwanafunzi mpya duniani, mkazi bora wa dunia nikitegemewa na waliowangu kuineemesha jamii kwa nguvu zangu , akili zangu, na vipaji nyangu. Wote waliniita mpendwa na mtoto mzuri huyu.

Sijui wale wote tuliozaliwa mwaka mmoja wangeandika wangesimulia vipi hadithi tamu ya wakati wa enzi za malaika na utukufu wa Mungu ukiwaangazia wakati ule hata bwana mkubwa Yesu aliosema , akiwaambia wenye uzoefu na dunia hii kuwa,msipoongoka na kuwa kama watoto wachanga hamtauriyhi ufalme wa Mungu.Enzi za kucheza na kufurahia kila kitu na kila mtu. Enzi za kubebwa na yeyote na kusanifiwa nayeyote.

Leo tuliozaliwa siku moja , mwaka mmoja wengine ni mabilionea, wengine ni wakubwa wa taasisi za umma au binafsi, wengine ni wasomi wazuoni wakubwa, wengine ni wahubiri wa injili wakiwaleta waliopote kwa Mungu, lakini wengine ni mafukara wakubwa , masikini waliokorea na wasiojiweza kwa lolote, wengine ni majambazi na wadokozi, wengine ni matapeli na wahuni mitaani na hasa wengine wanalala kwenye vipembezoni vya maduka makubwa. kwao usiku na mchana hakuna tofauti..Nabaki naduwaa na kujiuliza nini hasa hatima ya viumbe hawa walioletwa duniani bila kuingia mkataba baina yao na wazazi wao au baina yao na serikali zao kwamba kuja kwetu huko mliko mtuthibitishie neema na maisha ya raha.

Maisha kama walivyosema waswahili huenda ndivyo yalivyo. yanawagawanya binadanu bila wao kupenda na kuchukuliwa na upepo wa kila namna. hukumbwa na masahibu na kufanya yale yanayoweza kumwokoa.Hubadilika kutoka unadhifu wa kimalaika hadi mkanganyiko wa kidunia.Ndipo inapokuja suala la serikali. Kumlinda na kuwongoza huyu malaika mdogo ili afae duniani. kumlinda kutoka utoto hadi utu uzima na yeye kuwalinda na kuwasaidia wajao.

Naamini ni serikali tu yenye uwezo wa kuwalinda malaika hawa wadogo. kuwajengea mtizamo mzuri na kuwakabidhi nyenzo tamu za elimu, ufundi, nafasi kwa kipaji chake kila mmoja na kuondoka kuwaweka wote kundi moja kana kwamba dunia yote ni tambarare.

Tukiwa na serikali makini ya kuwajali raia wake tutakuwa tunapunguza majukumu ya kiserikali, wizara kwa ajili ya majambazi zinaweza kuondolewa.Linaloibua yote haya ni mfumo wa kuchuma wa dunia ambao kila alie na dhamana tamu hawaachii wanachi kilicho chao. hutumia fursa kuchuma yeye na kwa ajili ya kizazi chake hata cha tano. Ni silika ya dunia sasa watu wanataka kueneza nasaba katika nchi kuwa kama ndo nchi, wakipeana vijiti vya madaraka na ustaarabu nyuma ya nyumba kuwa dira ya nchi.

Ni wakati huu Marekani ingekumbuka Darfur, kongo,Somalia,na kwingineko. Lakini wananchi wa huko wamebaki hohehahe na serikali zao hazina habari, zimelala usingizi wa madaraka na shibe kuu ya minofu haramu ya cheo. Watu hawa leo wasingejuta kuzaliwa, maana kwao hakuna tofauti kuishi na kutokuishi.

Siku zote za maisha yangu ningetamani niione dunia na wale wanaokuja duniani wakifurahi kuwa wakazi wa dunia hii.siku zote wakijiandaa kuchukua majukumu mazito ya kufanya dunia eneo bora katika maeneo ya galax hili, ambano serikali zinawajibika kwa watu wao, wanachi wanacho cha kutoa kwa dunia na nchi zao na sisi tukiwa waumini wa dhehebu la dunia , tukizaliwa na kuingia katika kanisa na msikitiki wa dunia ya sayari yetu huku tukiimba nyimbo za ukombozi wa kiuchumi, maradhi, ubaguzi wa mali na ubabe wa kisiasa, tukilishwa neno la kuwajibika, kuchukia rushwa, uzembe, ufisadi, ujambazi na kwamba sisi ni watu tuliokuja kuhiji duniani, anga la dunia lingesheheni sauti za watu wenye nguvu, walioshiba kwa sababu watu wa jumba kuu si walafi, si walevi, si wachoyo na wamejitoa kwa akili na moyo kuwalisha wafuasi wa nchi neema ya dunia kwa hakika mbingu zingechungulia chini kuona maendeleo hayo na hapo ungekuwa mwanzo na enzi za miale mipya ya matumaini.

Magazeti yangeandika sifa katika vichwa vya habari, redio zingetangaza furaha kwa watu wote, na telesheni zingeonyesha watu waliojaa furaha na neema kuu.Maandamano yasingekuwa ya kulipua mabomu, mijeledi au fataki. Watu wangeandamana kusifu jumba kuu na watu wa jumba kuu,nao wangejiunga na umma na sasa lingekuwepo kundi moja , lenye mchungaji mmoja na wenye kusafiri pamoja.kinyume chake leo kuna makundi mengi tuu.kundi moja kila siku ni kuhanikiza sauti ya unisaidie, unisaidie na jingine ni kusidia pale panpobidi.

Natamani na nazidi kutamani kuwa wakazi wote wa dunia ni sawa, na mali ya dunia ni yao wote hivyo wenye dhamana ya kuitumia kwa manufaa ya umma tunawaomba wafanye hivyo.

Tunahitaji kuwa na kundi moja japo wengine kwenye kundi watakuwa warefu , wengine wafupi, wengine wanene, wengine wembamba wengine rangi tofauti lakini litakuwa kundi moja ambamo kila mmoja amridhika kuwa mwanakundi, na asiwepo mrefu kwa sababu kaiba urefu wa wengine, asiwepo mfupi kwa sababu kaiba ufupi wa wengine, asiwepo mnene kwa sababu kaiba unene wa wengine, asiwepo mwembamba kwa sababu kaiba wembamba wa wengine, na asiwepo mweupe kwa sababu kaibaweupewa wengine au mweusi kwa sababu kaiba weusi wa wengine na natamani siku zote za maisha yangu kuona kundi lote lina chakula, malazi mazuri,limesoma na kila mwanakundi ana rangi yake ya asili na siyo aliomwibia mwenzake na wote tukitoa sadaka kwa dunia iwe ipendezayo na yenye harufu kwa Mungu.

FIKRA MBADALA

Nashawishika kutamka kuwa kila kitu duniani kifanywacho na wanadamu na ikashindikana kukifanya kwa ufanisi wote , basi huwa kuna njia mbadala ya kufanya hivyo. Njia mbadala ni sehemu ya utaratibu wa kawaida ambao akili hulazimisha mwili kutenda hivyo ili kuondokana na kero ya tatizo lenyewe. Njia mbadala ni kiini cha kumaliza tatizo lakini ni sehemu tu ndogo ya ufumbuzi wa tatizo.

Duniani leo watu wanajadili habari ya kuwa na dunia mbadala, ambamo maadili , usafi, na uhuru wa kweli hupatikana, uchafuzi wa mazingira hakuna na hofu ya kutoboa utando wa hewa ya ozone hakuna. Ndipo inapokuja teknologia mbadala. Leo watu wanafikiria maisha mbadala, yenye nafuu ya kero, magonjwa, manyanyaso, umasikini na kila aina ya usaliti.

Serikali duniani zipo za mbadala, wengine wanaziita za mpito.shuleni kuna masomo mbadala, kuongezea pale palipopungua.kila kitu mbadala.

Ndipo nashawishika kuamini kuwa dunia ya leo inaongozwa na mawazo mbadala. watu wameshindwa kujua kiini cha matatizo ya dunia kwa sababu ya fikra mbadala.
Serikali hazitaki au zimeshindwa kuamua kwa kuzingatia matatizo halisi na kutumia njia halisi na wala siyo njia mbadala. unaposhindwa kupata hela kwa njia halali ndipo watu huuza miili, hubomoa nyumba za watu, huiba kwenye mabenki,na hufanya hivyo ikiwa njia mbadala ya kuondokana na matatizo yao. Wengine huchukua rushwa, hutoa hongo, na hata huua ili kuinusuru nafsi na tamaa zake za mali na utukufu wa utajiri kwa sababu akili ya kawaida imeshindwa kufikia kiini cha tatizo, na hivyo njia mbadala ni mauaji, uzandiki, ufisadi na kila aina ya uovu.

Kufikiri ni kazi, ni kazi kama kulima,au kufanya chochote unachotumia nguvu au akili. huchosha na mara nyingine huudhi kwa sababu ufikiricho huenda ni mlima mrefu sana. Wengi hatupendi kufikiri. Tukiwa tumeshindwa kwa sababu hatufikiri tunaamuaa kuchukua njia mbadala.

tunahitaji fikra pevu na siyi mbadala.

Njia mbadl

Tuesday, January 03, 2006

HAZINA PEVU

Hazina pevu, haiji kwa haraka haraka.Ni sehemu ya uvumilivu unaojikita katika kutafuta uimara na mhimili mkuu wa uang'avu wa akili.Ni sawa na embe dodo lililoiva. ukilila lingali bichi ni kama unameza klorokwini. Ukipata bahati ya kulilinua lilioiva mtini au ukalichuma mwenyewe mtini utadhani unameza vidonge vya magnezium, vinakupa unafuu nafsini na tumboni.

Hazina ya Tanzania si madini yanayochumwa na kutafutwa kwa udi na uvumba na wananchi pamoja na wawekezaji nchini, si mito, maziwa,mbuga au milima tuliokuwa tunaimba huko secondary na msingi kujivunia utajiri wetu, si mabonde na misitu lukuki iliojaa nyuki na wadudu wa kila aina, si chochote mungu alichotupa kionekanacho machoni na kisichooenekana katika uso wa ardhi bali ni hazina ya akili na fikra pevu za watu wa Tanzania.

Tunaweza kuwa na yote hayo na kwa sasa mwenyezi Mungu hakutunyima. Lakini kama hatuna maarifa, ujuzi, adabu ya akili na utulivu wa mipango tutabaki tukiwa na utajiri kwenye ramani ya nchi na vichwani mwetu isioonekana hadharani, au kuonekana kubadilisha maisha yawatu.

Kama ambavyo inachuka majira embe kuiva na kuonekana kufaa kuliwa ndivyo inavyochukua muda, nguvu, mali na ari na mali kuja kuwa na akili pevu kulisaidia taifa,.Kwa bahati mbaya Tanzania leo bado watu wanafikiri serikali yao tukufu inaweza kufanya au kuwafanyia maendeleo yao, la hasha, wananchi ndo wawe mbele kujipangia maendeleo yao ili kwa ujumla wake serikali iwasaidie kuweka mazingira huru na sawa katika kutumia utajiri wetu wa asili.

Kama serikali inakuwa na mipango ya maendeleo kwa muda kadhaa, kama ambavyo tuna dira ya 2025 ya kupunguza umaskini ndivyo hivyo kila mwananchi ajipangie dira yake atakavyotekeleza mipango yake ya muda mrefu na mfupi na aiambie serikali jinsi alivyoshindwa na kwa nini na ni wapi anahitaji msaada na siyo kulalamika tu bila kuchukua hatua yoyote ya kimaendeleo.

Twahitaji kurudi shule kupata upevu wa akili, shule yenyewe ni kutafuta maarifa popote ulipo, iwe kijijini au mjini, shuleni au nyumbani.

Hima watanzania na dunia , Dunia haitabadilika na kustaarabika zaidi na kuwa paradiso ndogo kama akili pevu na hazina mwanana ya nuru ya elimu, ujuzi, maarifa na ufundi havitatawala nyoyo za wakazi wa duniani.

Ni akili pevu tu na hazina zake ndizo zitakazoipa dunia na watu wake mwangaza na matumaini ya kuishi katika dunia ya ubabe wa fedha, silaha,na siasa za hali ya juu.

Akili pevu si wingi wa digrii na diploma , ni hali ya utambuzi wa mahitaji halisi ya dunia na watu wake na mchango chanya kwa kila tendo ulitendalo kwa dunia na watu wake kwa dhamana ndogo uliopewa na Mungu, watu, kikundi au familia.

Nashawishika kutamka kuwa wala rushwa, wezi, majambazi , wabaguzi wa rangi za ngozi ya miili yetu na ubaguzi mwingine wowote, wazembe kwa majukumu waliopewa,wasaliti, wote wanaangukia kwenye ukosefu wa akili pevu bila kujali idadi ya madarasa aliokaa shuleni.

Monday, January 02, 2006

HAZINA FIKRANI

Karibuni tujadili yahusuyo dunia. Yawapatayo binadamu wenye akili na utashi, lakini wenye hazina pevu fikrani kitika upembuzi mwanana. Ya binadamu na ubinadamu wake ni mengi. Husukumwa na ndoto, hisia, tamaa na husahau hazina ya kufikiri na nuru ya akili yake huangukia tamaani, nini hasa.....