Sunday, January 22, 2006

BARA LA GIZA

Isitoshe imekuwa ikinikera muda mrefu, kile kinachoitwa bara la giza , bara la Afrika.Kwa nini lilitwa hivyo na watu wa kaskazini mwa dunia.Jina la kejeli na lenye kila aina ya mzaa. labda kuzarau kilichokuwa Afrika au kwa vile watu wake inasemekana walikuwa wajinga kwa misingi ya akina mangungo wa msovero na kwingineko. Lakini somo la historia na kwenye vitabu dhalilishi vya historia ya maendeleo ya binadanu imebakia hivi kuwa Arika lilikuwa bara la giza.

Kwa misingi kwamba halikujulikana sana na watu wa kaskazini na kuwa shughuli za maendeleo ya binadamu yalikuwa nyuma sana. watu waliishi mapangoni, kwenye nyumba za full suti ya udongo ambazo bado zipo leo Afrika.

Au kwamba waliotumwa kutafuta unafuu wa makazi kwenye dunia isiyojulikana kama Amerika na Afrika waliwakuta watu wa maeneo hayo hawajui chochote kuhusu mabadiliko ya kijamii na kisayansi.Huenda ni kweli kwani akina Williamsoni wa Mwadui shinyanga walikuta wasukuma wa Tanzania wanachezea almasi, akaenda kwao Uingereza na kuja na groli za kuchonga na kubadilishana na almasi zilizotunzwa na wenyeji hao.

Williamsoni alikuwa maskini na kutoka ukoo maskini, baada ya kutajirika akataka kuoa kutoka ukoo wa malkia , lakini alikataliwa kutokana na historia yake, familia yake ilikuwa maskini tu. Akarudi Tanzania , akabadilisha maisha ya mwadui.Ilikuwa sehemu ndogo ya Tanzania yernye kila huduma.Wafanyakazi walipatiwa kila kitu, mkate, mayai, kilo mbili za nyama, mchele, bia , soda na mengine mengi hata maisha yalipobadilika watu hawa leo ni maskini.Hawakuweka akiba , walijua maisha ndo hayo hayatabadilika. imebakia historia nzuri ya kula mayai na mikate.

Wazungu walipora utajiri wetu.Juzi nilikuwa kwenye mji mdogo wa Geita mkoani mwanza kaskazini mwa Tanzania, nilikutana na rafiki yangu mmoja .Tuliongea mengi lakini mwishowe aliniuliza unajua maana ya jina hili GEITA.Nikamwambia hapana. Akanambia kuwa geita ni neno la kizungu.Hapo mgodi wa dhahabu wa geita upo leo wazungu waingereza walichimba zamani na wakagundua kuwa eneo lote la wilaya hiyo ni dhahabu tupu, wakaamua kuliita ''Gold Environment in Tanganyika'' kwa kifupi GEITA. akazidi kunambia kuwa dhahabu ya geita ndo imependezesha London.

Lakini napata hamasa kuu ya kuwa bara la giza lilizipamba Ulaya. Misaada inayopatikana kutoka ulaya ni ziada na faida ya mtaji kutoka Afrika.Viongozi wa Afrika wanapoenda Kaskazini kuomba misaada, siyo misaaada ni kuomba sehemu ya faida ya mtaji wetu ulioporwa.

Nahitaji kuungwa mkono hapa au kupingwa kuwa lazima Afrika leo iwe na hisa katika IMF na WB kwani uchumi wake uliporwa na wazungu kwa lugha isiyo na haya naweza kusema waliiba utajiri Afrika wakitumia ukarimu wa babu zetu.

Afrika halikuwa bara la giza na wala haijawahi kutokea hivyo.Siku zote kaskazinin hutafuta maneno na misamiati ya kupumbaza waafrika.Afrika imekuwa ikikua kwa kasi ukweli ni kwamba mtoto Afrika alichelewa kukua kwa sababu alidekezwa sana na wazazi wake na kwamba walikuwa matajiri kupindukia, hivyo hakuwa na haraka ya kukimbia kimbia ajitegeee
na kuwahi kutafuta mali. Mtoto Ulaya aliwahi kutembea sana, ilikuwa hivyo kwa sababu ya matatizo yake , alikuzwa hivyo ili ajitegemee mapema maana mazingira yake yalikuwa magumu.Hakuwa na ardhi kubwa na pana, yenye rutuba nk.Hivyo kwa ukorofi wake akamwibia ndugu yake Afrika na kuanza kumwuita mjinga na eti yuko gizani.

Mali ya duni a ni ya wote.Lakini linalonishangaza ni kuwa mpaka leo waafrika tunapigana, hatupendani, serikali hazisaidii watu wake, viongozi wetu wanaenda parisi club, IMF,WB na kwingineko kuomba msaada.Wanawaita wawekezaji kuchuma na kuendeleza Waafrika, wanaambiwa ili kuwa na msaada lazima kuwe na utawala bora, haki za binadamu, uwazi kana kwamba sisi bado tuko gizani. La kunishangaza tunaitikia tu kwani tukikataa tutanyimwa misaada.

Ukikataa masharti ya kaskazini unawekewa vikwazo vya kimataifa, vikwazo vya kiuchumi.Ni nini tumemkosea Mungu sisi Afrika na waafrika kwamba uchumi uliojenga ulaya ulitoka Afrika lakini sisi sasa wenye uchumi huo hatuwezi kuutumia kubadilisha maisha na mustakabali wa waafrika wote?Nani au mzazi gani wa Afrika alitenda dhambi hii kubwa ambayo haiwezi kusamehewa nasi tukajenga kujiamini na kizazi hiki kikasomga mbele kwa mbwembwe kama ambavyo kaskazini ilivyo? kwa nini hatuwezi.

Twahitaji kuona ulaya ikija afrika kuomba mali ya Afrika na siyo kuja kutawala Afrika kwa misingi ya mashirika ya fedha n.k

Nitazidi kukataa na kushawishika kuwa Afrika hakuna giza- na wala haijatokea hivyo badala yake giza la ulaya walilileta Afrika na kufanya afrika itiwe huzuni na kubakia hivyo mpaka leo.
Afrika ni mwanga na imekuwa nguzo ya kiuchumi ya dunia mpakam sasa ,Je ni kwa nini tusijenge na kujenga historia yetu ya matumaini kuliko hii ya ulaya ya giza ?
ni wapi lilitendeka kosa?

2 Comments:

Blogger Ndesanjo Macha said...

Swali lako mwishoni mwa makala hii nimeondoka nalo: kwanini tusijenge historia ya Afrika yenye matumaini?

Tuna uwezo wa kuanza kuandika historia yetu kwa kutumia blogu zetu maana historia yetu imeandikwa kidogo sana. Sehemu kubwa ya historia yetu ambayo imeandikwa na wazungu ni "historia ya afrika kwa mujibu wa mzungu." Wao ndio wanaandika vitabu vya historia yao na wao pia ndio wanaoandika vitabu vya historia yetu!

11:01 PM  
Blogger myslot said...

ดูฟรีไม่มีเบื่อ ดูหนังออนไลน์ Alita: Battle Angel อลิตา แบทเทิล แองเจิ้ล (2019) หนังใหม่ล่าสุด หนังเต็มเรื่องชัดสุดๆ

https://www.doonung1234.com/

2:34 AM  

Post a Comment

<< Home