Tuesday, January 17, 2006

SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU

Nilipozaliwa miaka mingi iliopita, sikujua ni wapi naelekea na ni wapi natoka. ningali mdogo niliiona dunia nzuri sana maana ilikuwa dunia isyokuwa na majukumu, badala yake mimi nilikuwa naidai dunia, maana ilikuwa ni lazima nile, nivae, nilale kuzuri, nitibiwe, nisome au nisomeshwe, nipendwe na watu wangu kunijali kama mtoto na ndugu yao mpendwa.

Nilikuwa zao jipya duniani, mali mpya mnadani na mwanafunzi mpya duniani, mkazi bora wa dunia nikitegemewa na waliowangu kuineemesha jamii kwa nguvu zangu , akili zangu, na vipaji nyangu. Wote waliniita mpendwa na mtoto mzuri huyu.

Sijui wale wote tuliozaliwa mwaka mmoja wangeandika wangesimulia vipi hadithi tamu ya wakati wa enzi za malaika na utukufu wa Mungu ukiwaangazia wakati ule hata bwana mkubwa Yesu aliosema , akiwaambia wenye uzoefu na dunia hii kuwa,msipoongoka na kuwa kama watoto wachanga hamtauriyhi ufalme wa Mungu.Enzi za kucheza na kufurahia kila kitu na kila mtu. Enzi za kubebwa na yeyote na kusanifiwa nayeyote.

Leo tuliozaliwa siku moja , mwaka mmoja wengine ni mabilionea, wengine ni wakubwa wa taasisi za umma au binafsi, wengine ni wasomi wazuoni wakubwa, wengine ni wahubiri wa injili wakiwaleta waliopote kwa Mungu, lakini wengine ni mafukara wakubwa , masikini waliokorea na wasiojiweza kwa lolote, wengine ni majambazi na wadokozi, wengine ni matapeli na wahuni mitaani na hasa wengine wanalala kwenye vipembezoni vya maduka makubwa. kwao usiku na mchana hakuna tofauti..Nabaki naduwaa na kujiuliza nini hasa hatima ya viumbe hawa walioletwa duniani bila kuingia mkataba baina yao na wazazi wao au baina yao na serikali zao kwamba kuja kwetu huko mliko mtuthibitishie neema na maisha ya raha.

Maisha kama walivyosema waswahili huenda ndivyo yalivyo. yanawagawanya binadanu bila wao kupenda na kuchukuliwa na upepo wa kila namna. hukumbwa na masahibu na kufanya yale yanayoweza kumwokoa.Hubadilika kutoka unadhifu wa kimalaika hadi mkanganyiko wa kidunia.Ndipo inapokuja suala la serikali. Kumlinda na kuwongoza huyu malaika mdogo ili afae duniani. kumlinda kutoka utoto hadi utu uzima na yeye kuwalinda na kuwasaidia wajao.

Naamini ni serikali tu yenye uwezo wa kuwalinda malaika hawa wadogo. kuwajengea mtizamo mzuri na kuwakabidhi nyenzo tamu za elimu, ufundi, nafasi kwa kipaji chake kila mmoja na kuondoka kuwaweka wote kundi moja kana kwamba dunia yote ni tambarare.

Tukiwa na serikali makini ya kuwajali raia wake tutakuwa tunapunguza majukumu ya kiserikali, wizara kwa ajili ya majambazi zinaweza kuondolewa.Linaloibua yote haya ni mfumo wa kuchuma wa dunia ambao kila alie na dhamana tamu hawaachii wanachi kilicho chao. hutumia fursa kuchuma yeye na kwa ajili ya kizazi chake hata cha tano. Ni silika ya dunia sasa watu wanataka kueneza nasaba katika nchi kuwa kama ndo nchi, wakipeana vijiti vya madaraka na ustaarabu nyuma ya nyumba kuwa dira ya nchi.

Ni wakati huu Marekani ingekumbuka Darfur, kongo,Somalia,na kwingineko. Lakini wananchi wa huko wamebaki hohehahe na serikali zao hazina habari, zimelala usingizi wa madaraka na shibe kuu ya minofu haramu ya cheo. Watu hawa leo wasingejuta kuzaliwa, maana kwao hakuna tofauti kuishi na kutokuishi.

Siku zote za maisha yangu ningetamani niione dunia na wale wanaokuja duniani wakifurahi kuwa wakazi wa dunia hii.siku zote wakijiandaa kuchukua majukumu mazito ya kufanya dunia eneo bora katika maeneo ya galax hili, ambano serikali zinawajibika kwa watu wao, wanachi wanacho cha kutoa kwa dunia na nchi zao na sisi tukiwa waumini wa dhehebu la dunia , tukizaliwa na kuingia katika kanisa na msikitiki wa dunia ya sayari yetu huku tukiimba nyimbo za ukombozi wa kiuchumi, maradhi, ubaguzi wa mali na ubabe wa kisiasa, tukilishwa neno la kuwajibika, kuchukia rushwa, uzembe, ufisadi, ujambazi na kwamba sisi ni watu tuliokuja kuhiji duniani, anga la dunia lingesheheni sauti za watu wenye nguvu, walioshiba kwa sababu watu wa jumba kuu si walafi, si walevi, si wachoyo na wamejitoa kwa akili na moyo kuwalisha wafuasi wa nchi neema ya dunia kwa hakika mbingu zingechungulia chini kuona maendeleo hayo na hapo ungekuwa mwanzo na enzi za miale mipya ya matumaini.

Magazeti yangeandika sifa katika vichwa vya habari, redio zingetangaza furaha kwa watu wote, na telesheni zingeonyesha watu waliojaa furaha na neema kuu.Maandamano yasingekuwa ya kulipua mabomu, mijeledi au fataki. Watu wangeandamana kusifu jumba kuu na watu wa jumba kuu,nao wangejiunga na umma na sasa lingekuwepo kundi moja , lenye mchungaji mmoja na wenye kusafiri pamoja.kinyume chake leo kuna makundi mengi tuu.kundi moja kila siku ni kuhanikiza sauti ya unisaidie, unisaidie na jingine ni kusidia pale panpobidi.

Natamani na nazidi kutamani kuwa wakazi wote wa dunia ni sawa, na mali ya dunia ni yao wote hivyo wenye dhamana ya kuitumia kwa manufaa ya umma tunawaomba wafanye hivyo.

Tunahitaji kuwa na kundi moja japo wengine kwenye kundi watakuwa warefu , wengine wafupi, wengine wanene, wengine wembamba wengine rangi tofauti lakini litakuwa kundi moja ambamo kila mmoja amridhika kuwa mwanakundi, na asiwepo mrefu kwa sababu kaiba urefu wa wengine, asiwepo mfupi kwa sababu kaiba ufupi wa wengine, asiwepo mnene kwa sababu kaiba unene wa wengine, asiwepo mwembamba kwa sababu kaiba wembamba wa wengine, na asiwepo mweupe kwa sababu kaibaweupewa wengine au mweusi kwa sababu kaiba weusi wa wengine na natamani siku zote za maisha yangu kuona kundi lote lina chakula, malazi mazuri,limesoma na kila mwanakundi ana rangi yake ya asili na siyo aliomwibia mwenzake na wote tukitoa sadaka kwa dunia iwe ipendezayo na yenye harufu kwa Mungu.


8 Comments:

Blogger boniphace said...

Bwire nakubali kabisa umenikumbusha niliowahi kusoma nao niliwao kucheza nao chandimu na kadhalika. Wengine afadhali walishatutoka maana wamechagua usingizi bora lakini tuliobaki hata hatuonani, Tunatamani tukikutana tunyweshane sumu! Mungu bariki wanao kazi inaendelea

9:06 AM  
Blogger Jeff Msangi said...

Karibu sana Bwire.Uwanjani ndio hapa,ngoma ndio hii au kabumbu ndio imeanza tu,dakika tisini ni nyingi kumaliza.Tupo pamoja katika ukombozi wa fikra.

11:19 AM  
Blogger Ndesanjo Macha said...

Bwire, ni furaha ilioje kukukaribisha ndugu yetu. Tena umekuja kwa kauli nzito sana. Umesema kuwa katika dunia hii yote tisa, kumi ni akili na fikra. Ukaongeza kuwa akili na fikra pevu havina uhusiano wowote na digrii au diploma. Hapo umenikuna sana. Karibu.

1:28 AM  
Blogger mloyi said...

Karibu, Uwanja upo wazi.Karibu.

8:52 AM  
Blogger FOSEWERD Initiatives said...

bwire karibu sana. wewe ni hazina kubwa ya mawazo. kizuri zaidi unafikiria kwa sauti na wote tumekusikia, tunakusikia kabumbu na lisonge mbele. jisikie uko nyumbani na kiu yako sasa itakatika!

10:36 AM  
Blogger Innocent Kasyate said...

Karibu bwana Bwire sana.usiache kupitia globuni kwangu pia.

10:17 PM  
Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

9:49 AM  
Blogger peri kızı said...


With the latest Turkish sex anal porno To get the most out of this platform visit our website. Sex porns

10:35 AM  

Post a Comment

<< Home